IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Miji Ambayo ina muda mrefu zaidi na muda mfupi zaidi wa kufunga Mwezi wa Ramadhani

18:11 - March 07, 2023
Habari ID: 3476674
TEHRAN (IQNA)-Ripoti ya hivi imebaini miji ya dunia ambako Waislamu hufunga saa nyingi zaidi na wale ambao hufunga saa chache zaidi.

Mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa mfungo, unatarajiwa kuanza Alhamisi, Machi 23, na kumalizika Alhamisi, Aprili 20.

Katika nchi za Kiislamu za eneo, urefu wa wastani wa siku ya kufunga ni kama masaa 15.

Katika ulimwengu wa Kiarabu, Visiwa vya Comoro vitakuwa na idadi ndogo zaidi ya masaa ya kufunga. Waislamu huko watafunga kwa takriban masaa 12 na dakika 37.

Hii ni wakati saa za siku nchini Algeria na Tunisia zitafikia saa 15 na dakika 45.

Buenos Aires nchini Argentina na Johannesburg nchini Afrika Kusini zina muda wa kufunga duniani; kati ya saa 12 na 32.

Puerto Montt, Chile na Christchurch, New Zealand ina muda mfupi zaidi wa kufunga duniani ambapo Waislamu huko kufunga masaa 11-12 kwa siku.

Kuhusu muda mrefu zaidi wa kufunga, miji ya Ulaya inashikilia rekodi hiyo ambapo mji wa Warsaw nchini Poland na Moscow nchini Russia ikifunga kwa zaidi ya saa 18.

Ramadhani ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu. Ni kipindi cha sala, saumu, utoaji wa sadaka na uwajibikaji kwa Waislamu duniani kote.

4126463

Habari zinazohusiana
Kishikizo: ramadhani
captcha