IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Qari wa Iran ashinda Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Televisheni ya Al-Kawthar

10:27 - April 11, 2024
Habari ID: 3478668
IQNA – Mashindano ya 17 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Kanali ya Televisheni ya Al-Kawthar yamemalizika tamati, huku qari wa Iran Ustadh Mostafa Hemmat Qassemi akishinda tuzo ya juu zaidi.

Hemmat Qassemi alipata jumla ya pointi 87.25 na kuwa wa kwanza kwenye kinyang'anyiro hicho. Mshindi wa pili alikuwa Mostafa Heidari kutoka Afghanistan kwa pointi 86.5, huku Muhammad Ridha al-Haj Awman kutoka Indonesia akishinda nafasi ya tatu kwa pointi 86.25.

Nafasi ya nne na ya tano ilikwenda kwa Abdul Hussain Suwaidan kutoka Ujerumani na Hassan Shakir Hamoud al-Saedi kutoka Iraq, mtawalia.

Washiriki watano bora walikuwa wameshindana katika fainali kuu, iliyofanyika usiku uliobarikiwa wa mkesha wa Idul-Fitr.

Mashindano hayo ya Qur'ani Tukufu Televisheni ya Al Kawthar yanayofanyika kwa njia ya mawasiliano ya intaneti yamepewa anuani ya "Inna lil-Muttaqina Mafaza" (Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu- Quran Tukufu, Surat An Nabaa  aya ya 31)  na hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ni mashindano makubwa zaidi ya ulimwengu ya Kiislamu ya usomaji wa Qur'ani moja kwa moja kwa njia ya televisheni yanayorushwa na Al-Kawthar, Televisheni ya lugha ya Kiarabu ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB).

3487894

captcha