IQNA

Hija

Zaidi ya Wairani 83,000 kushiriki ibada ya Hija mwaka huu

11:20 - April 23, 2024
Habari ID: 3478723
IQNA - Zaidi ya Wairani 83,000 wataelekea Saudi Arabia kushiriki katika ibada ya Hija mwaka huu, afisa mmoja alisema.

Seyed Abbas Hosseini Mkuu wa Shirika la Hija na Ziyara za Kidini Iran ametoa kauli hiyo katika kikao cha kupanga na kuratibu kilichohudhuriwa na maafisa wa Hija wa Iran akiwemo mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya Hija na Ziyara za Kidini Hujjatul Islam Abdul Fattah Navab. Hosseini alisema kuwa mchakato wa kupata visa kwa mahujaji wa Iran umeanza.

Zaidi ya hayo, mkuu wa masuala ya matibabu kwa ajili ya Hija, Ali Mar’ashi, alisema kuwa maafisa wa afya wamethibitisha uwezo bora wa kiafya  wa watu 82,164 waliojiandikisha kwenda Hija huku uchunguzi ukiendelea kwa waliosalia amapo  watu 143 hawajaweza kupata idhini ya kimatibabu kuhudhuria Hijja.

Mwaka jana, takriban Wairani 85,000 walishiriki katika ibada ya Hija, na kuashiria kupanda kwa 114% ikilinganishwa na mwaka uliotangulia ambao ulikuwa na vikwazo kutokana na janga la corona.

Kila mwaka, isipokuwa kwa miaka ambayo idadi ya mahujaji ilipunguzwa kwa sababu ya janga la coronav, karibu Waislamu milioni tatu kutoka ulimwenguni kote hukusanyika katika mji mtakatifu wa Makkka, Saudi Arabia, kwa ajili ya ibada ya Hija  kila mwaka.

Hija ni safari ya kwenda Makka ambayo kila Mwislamu mwenye uwezo wa kimwili na uwezo wa kifedha analazimika kuitekeleza angalau mara moja katika maisha yake.

Hija ya kila mwaka inachukuliwa kuwa moja ya nguzo za Uislamu na ni mjumuiko mkubwa zaidi wa aina yake duniani.

Pia ni dhihirisho la umoja wa Waislamu na kujisalimisha kwao kwa Mwenyezi Mungu.

 4213343

Kishikizo: hija iran
captcha