IQNA

Idul Fitr

Idul Fitr : Siku ya Kupokea Malipo Baada ya Saumu ya Ramadhani

13:49 - April 10, 2024
Habari ID: 3478663
IQNA - Ramadhani, mwezi wa ibada na kujitolea, unafikia kilele kwa Waislamu kujiandaa kupokea malipo yao kutoka kwa Mwenyezi Mungu baada ya mwezi wa saumu na ibada.

Siku ya kwanza ya Shawwal, mwezi unaofuata baada ya Ramadhani, inayojulikana kama "Idul Fitr Fitr" miongoni mwa Waislamu, inaashiria kuzaliwa upya kiroho. Siku hii, Mwislamu ambaye amefunga kwa mwezi mmoja hutakaswa na kundolewa dhambi, na kurudi kwenye asili yake iliyotakasika. Katika siku ya Idul Fitr saumu imeharamishwa, na ni wajibu kwa wenye uwezo  kutoa Zakat ul Fitr.

Kwa hakika  Idul Fitr ni siku ya furaha tele kwa waumini, kwani kila Muislamu anahisi hali ya utimilifu katika kukamilisha wajibu wake kama alivyoamurishwa na Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, pia ni siku ya kutazamia na kuwa na wasiwasi, kwani waumini huwa wanasubiri huku  ya Mwenyezi Mungu kuhus amali zao za mwezi mzima na thawabu watakazopokea.

Idul Fitr ni siku ambayo Waislamu hupokea malipo ya mwezi wa Ramadhani. Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) amenukuliwa katika iliyopokewa na Jabir ibn Abdullah Ansari akisema kwamba katika siku ya kwanza ya Shawwal, Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaita waumini, akiwahimiza kupokea malipo yao.

Isitoshe, mkesha wa Idul Fitr, unaojulikana pia kama usiku wa zawadi, ni wakati maalum. Mtume Muhammad (SAW) alisema kuwa katika usiku huu, Mwenyezi Mungu huwalipa wale wanaoabudu malipo yasiyo na kifani na inapoingia siku ya Idi, Malaika hushuka duniani, wakisimama barabarani na kwenye njia, wakiita Umma wa Muhammad kujiunga na Swala ya Idi kwa ajili ya kupokea malipo mengi na msamaha wa dhambi kubwa.

Tunapoadhimisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kutarajia furaha katika Sikukuu ya Idul Fitr, ni wakati mzuri wa kuomba msamaha wa dhambi zetu na kujitahidi kustahiki thawabu kuu za Mwenyezi Mungu.

3487877

captcha