IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Qari wa Iran asema Shindano la Qur’ani ya Saudi lilikuwa ngumu sana

14:18 - April 10, 2023
Habari ID: 3476843
TEHRAN (IQNA) – Yunes Shahmoradi kutoka Iran aliyeshika nafasi ya kwanza katika Toleo la 2 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Otr Elkalam nchini Saudi Arabia amesema shindano hilo lilikuwa la kiwango cha juu.

 Akizungumza na IQNA baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini (RA) mjini hapa, aliyataja mashindano hayo kuwa ni miongoni mwa mashindano magumu zaidi ya Qur'ani Tukufu duniani kushinda.

Alisema si kama mashindano ya Iran au Malaysia ambayo yanajumuisha mtindo wa Taqhiqh wa qiraa kwani washiriki wa shindano la Otr Elkalam wanapaswa pia kuwa na uwezo wa qiraa ya Tarteel.

Amesema inajulikana kuwa usomaji wa Tarteel uko katika kiwango cha juu katika nchi kama Saudi Arabia na Moroko na hii inafanya kuwa ngumu sana kushinda shindano hilo.

Shahmoradi pia alibainisha kuwa hakuna kizuizi chochote cha ushiriki wa maqari katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Otr Elkalam na idadi kubwa ya maqari kutoka nchi mbalimbali walishiriki katika mashindano hayo.

"Kwa vile Seyed Jasem Mousawi kutoka Iran alishiriki katika (toleo la kwanza) mwaka jana na kuchukua nafasi ya nne, niliamua pia kushiriki katika tukio la Qur'ani mwaka huu na, namshukuru Mwenyezi Mungu, nilipata uwepo wa mafanikio."

Alipoulizwa kuhusu nukta zilizomsaidia kushinda tuzo ya kwanza, msomaji huyo wa Iran alisema kwanza ilikuwa ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kisha kuiga mtindo wa usomaji wa Qur'ani wa marehemu qari wa Misri Sheikh Muhammad Rifat.

Pia alibainisha kuwa mashindano hayo yalifanyika katika hatua saba, ambapo tatu za kwanza ziliandaliwa mtandaoni na zilizosalia ana kwa ana nchini Saudi Arabia.

Aidha amesema hajui kama kuboreka uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia hivi karibuni kuliathiri mafanikio yake katika mashindano hayo.

Iranian Qari Says Saudi Arabia’s Otr Elkalam Int’l Quran Contest among Most Difficult to Win

Shahmoradi alipokea zawadi ya fedha taslimu riyal milioni tatu za Saudia au USD 800,000 kwa kuchukua nafasi ya kwanza katika kitengo cha usomaji wa Qur'ani.

Wengine watatu walioingia fainali katika kitengo hiki walikuwa Abdul Aziz Faqih kutoka nchi mwenyeji aliyemaliza mshindi wa pili na Wamorocco Zakariya al-Zirak na Abdullah Al-Dughri waliibuka wa tatu na wa nne mtawalia.

Shindano hilo liliianza siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani (Machi 23).

Waandalizi wanasema moja ya malengo yao yalikuwa ni kuangazia wingi wa tamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu, kupitia kusoma Qur'ani Tukufu na Adhana..

Mwaka huu, shindano hilo lilivutia washiriki 50,000 Waislamu kutoka zaidi ya nchi 100, wote wakiwania kufuzu.

Kati ya washiriki 2,116 walioshinda, washiriki 36 (18 katika qiraa au usomaji Qur'ani na 18 katika adhana) walifuzu kwa hatua za mwisho.

Jumla ya pesa za tuzo za shindano hilo zilizidi riyal milioni 12 za Saudi ($ 3.2 milioni).

3483127

captcha