IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Msikiti Mkuu wa Makka kuandaa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Saudia

15:50 - May 04, 2023
Habari ID: 3476955
TEHRAN (IQNA) –Mashindano ya 43 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Saudi Arabia yatafanyika katika mji mtakatifu wa Makka msimu huu wa joto.

Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Okaz, Msikiti Mkuu wa Makkah (Masjid al Haram) utakuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya  Qur'ani katika mwezi wa Hijri wa Safar (Agosti-Septemba).

Wizara ya Masuala ya Kiislamu, Dawah, na Mwongozo kila mwaka huandaa mashindano ya usomaji, kuhifadhi na tafsiri ya Qur'ani Tukufu.

Waziri wa Masuala ya Kiislamu Abdul Latif Al Sheikh alisema mashindano hayo yana hadhi kuu kimataifa.

Ameongeza kuwa, lengo lake ni kukuza mafunzi ya usomaji, kuhifadhi na kufasiri Qur'ani Tukufu miongoni mwa vijana wa Kiislamu.

Kuhifadhi Qur'ani nzima na usomaji katika mbinu zote saba za usomaji pamoja na uzingatiaji wa sheria za Tajweed, na tafsiri ya aya, na kuhifadhi Juzuu 15 za Qur'ani ni miongoni mwa kategoria za kimataifa za mashindano hayo. Taarifa kuhusu masharti ya kushiriki katika shindano hili zinapatikana kwa Kiarabu na Kiingereza kwenye tovuti ya sekretarieti ya mashidano.

4138483

captcha