iqna

IQNA

saudi arabia
Vita vya Yemen
TEHRAN (IQNA)- Saudi Arabia imeripotiwa kulijulisha linalojiita baraza la uongozi wa rais wa Yemen juu ya uamuzi wa kusitisha vita haribifu nchini Yemen baada ya miaka minane ya uchokozi.
Habari ID: 3476834    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/08

Mashindano ya Qur'ani
TEHRAN (IQNA) – Yunes Shahmoradi kutoka Iran ameibuka mshindi katika toleo la pili la Shindano la Kimataifa la Qur’ani Tukufu la Otr Elkalam nchini Saudi Arabia.
Habari ID: 3476831    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/08

Ajali
TEHRAN (IQNA) – Takriban waumini 20 waliokuwa katika hija ndogo ya Umrah wamepoteza Maisha na wengine 29 kujeruhiwa wakati basi lililokuwa limewabeba lilipopinduka na kuwaka moto katika eneo la Aqaba Shaar kusini mwa mkoa wa Asir, Saudi Arabia Jumatatu alasiri.
Habari ID: 3476774    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/28

Mwezi wa Ramadhani
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Saudi Arabia imetangaza kuzndia kampeni mpya ya kupunguza kiwango cha israfu ya chakula ambayo imetajwa kuwa tatizo sugu katika nchi hiyo tajiri ya Kiarabu.
Habari ID: 3476769    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/27

Mashindano ya Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA) – Televisheni ya MBC ya Saudi Arabia imeanza kutangaza mfululizo wa pili wa mashindano ya kimataifa ya usomaji wa Qur'ani Tukufu na Adhana.
Habari ID: 3476756    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/25

Sera za Kigeni Iran
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametangaza kuwa, atakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia mnamo siku chache zijazo na akasema: "tulikubaliana kuwa jumbe za kiufundi za pande zote mbili zitembelee balozi na balozi ndogo na kufanya maandalizi ya kivitendo ya kufunguliwa tena balozi hizo."
Habari ID: 3476727    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/19

Mwezi wa Ramadhani
TEHRAN (IQNA) – Maafisa wa Saudi Arabia wanasema zaidi ya lita milioni 40 za maji ya Zamzam zitasambazwa katika Msikiti Mkuu wa Makka (Masjid al-Haram) miongoni mwa Mahujaji katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3476720    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/17

Uhusiano wa nchi za Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesisitiza stratejia isiyobadilika ya sera za nje za Jamhuri ya Kiislamu kuhusu ushirikiano wa pande zote, endelevu na wenye manufaa na majirani zake na kusema: ili kuondokana na changamoto zilizopo ambazo kuendelea kwake hakuna maslahi kwa nchi yoyote katika eneo hili, ni lazima ushirikiano na mshikamano vichuke nafasi ya mifarakano na uhasama.
Habari ID: 3476719    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/17

Ulimwengu wa Kiislamu
TEHRAN (IQNA)-Mhadhiri mwenye makao yake nchini Uingereza anasema Washington na Tel Aviv "zilishangazwa" baada ya Tehran na Riyadh kutangaza kuanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia siku ya Ijumaa.
Habari ID: 3476698    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/12

Ulimwengu wa Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Makundi mbalimbali ya kieneo yamekaribisha makubaliano ya kurejesha tena uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Ufalme wa Saudi Arabia.
Habari ID: 3476692    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/11

Ulimwengu wa Kiislamu
TEHRAN (IQNA)-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia zimefikia makubaliano ya kurejesha uhusiano wao wa kidiplomasia na kufungua tena balozi, miaka saba baada ya kuvunjika uhusiano huo kutokana na masuala kadhaa.
Habari ID: 3476685    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/10

Umrah
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi iliweka jumla ya mahujaji wa kigeni wanaofanya Hija ndogo ya Umra tangu mwanzo wa huu wa Kiislamu ni milioni 4.8.
Habari ID: 3476571    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/16

Ajali ya Winchi
TEHRAN (IQNA) - Mahakama ya Saudia imetoa uamuzi wa ajali ya winchi iliyotokea mwaka 2015 katika Msikiti Mkuu wa Makka ambayo iliua takriban watu 109.
Habari ID: 3476565    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/15

Maonyesho ya Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA) - Banda la Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia lilikabidhi nakala 30,000 za Qur'ani Tukufu miongoni mwa wageni katika Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo.
Habari ID: 3476504    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/02

Hali ya Waislamu Saudia
TEHRAN (IQNA) – Matumizi ya vipaza sauti katika misikiti kote Saudi Arabia yatawekewa vikwazo, kulingana na Wizara ya Masuala ya Kiislamu, Wito na Mwongozo.
Habari ID: 3476436    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/20

Siasa za Saudia
TEHRAN (IQNA)- Taarifa zinasema mhubiri mmoja mashuhuri nchini Saudi Arabia amehukumiwa kunyongwa katika kile kinachoongokana ni ukandamizaji dhidi ya wanaopinga sera za Ufalme huo.
Habari ID: 3476408    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/15

Wanawake Saudia
TEHRAN (IQNA) – Wanawake wameruhusiwa kuendesha treni zinazosafiri kati ya miji mitakatifu ya Makka na Madina nchini Saudi Arabia.
Habari ID: 3476350    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/03

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu/13
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Mustafa Muslim (1940-2021) alikuwa mtu mashuhuri katika uwanja wa sayansi za Qur’ani ambaye aliandika vitabu 90, ikiwa ni pamoja na ensaiklopidia za sayansi za Qur’ani.
Habari ID: 3476346    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/02

Mafuriko Saudia
TEHRAN (IQNA)- Mafuriko makubwa yalikumba mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia siku ya Ijumaa asubuhi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku, kuharibu magari na mali katika mji huo.
Habari ID: 3476292    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/23

Vita vya Saudia dhidi ya Yemen
TEHRAN (IQNA) – Ujumbe kutoka Oman uko katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a, kufanya mazungumzo na wanachama wa ngazi za juu wa harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Ansarullah kuhusu kurefusha usitishaji vita unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa nchini Yemen.
Habari ID: 3476286    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/22