IQNA

Waislamu Marekani

Tahariri ya kichochezi ya gazeti la WSJ yaibua taharuki Marekani

23:01 - February 04, 2024
Habari ID: 3478304
IQNA - Polisi wameimarisha doria katika nyumba za ibada na "vituo vikuu vya miundombinu" huko Dearborn, jimbo la Michigan nchini Marekani.

Tawi la Michigan la Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR-MI) siku ya Jumamosi lilikaribisha hatua hiyo, ambayo ilikuja baada ya Jarida la Wall Street Journal (WSJ) kuchapisha maoni ya uchochezi dhidi ya Uislamu yanayolenga jiji hilo.

Meya wa Dearborn Abdullah Hammoud alisema ulinzi uliimarishwa kufuatia tahariri ya  WSJ yenye kichwa, "Welcome to Dearborn, America's Jihad Capital,"  yaani ‘Karibuni Dearborn, Mji Mkuu wa Jihad Marekani,” ambapo mwandishi alitoa madai ya uongo kuwa eti waandamanaji wanaounga mkono Palestina pia wanaunga mkono ugaidi.

Makala hiyo ya kichochezi iliandikwa na Steven Salinski, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Vyombo vya Habari ya Mashariki ya Kati yenye makao yake Washington, D.C., taasisi ambayo imeelezwa kuwa ni "kundi linalopinga Uislamu."

"Tunakaribisha hatua chanya iliyochukuliwa na Meya Hammoud kulinda jumuiya ya Kiislamu dhidi ya mashambulizi yanayoweza kutokea kulingana na madai ya uongo katika makala isiyo usio sahihi na wa uchochezi," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa CAIR-MI, Dawud Walid. "Wale wanaounga mkono mauaji ya kimbari na mauaji ya kikaumu huko Gaza sasa wanatumia mbinu za kupaka matope ili kuwazuia Wamarekani kujifunza ukweli kuhusu vitendo vya kikatili vya serikali ya mrengo wa kulia ya Israel inayolenga watu wa Palestina."

CAIR, yenye makao yake Washington, D.C., hivi majuzi ilitoa data mpya ya haki za kiraia inayoonyesha kwamba imepokea malalamiko 3,578 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ya 2023 huku kukiwa na wimbi linaloendelea la chuki dhidi ya Uislamu na Palestina.

Hii inawakilisha ongezeko la asilimia 178 ya vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu  katika miezi mitatu ya mwisho ya 2023 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

3487075

captcha