IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya 24 ya Qur’ani ya Bint Maktoum yamalizika UAE

20:16 - January 25, 2024
Habari ID: 3478252
IQNA – Toleo la 24 la Mashindano ya Qur’ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) yalihitimishwa katika hafla iliyofanyika mjini Dubai.

Jumuiya ya Wanawake ya An-Nahdha ya Dubai iliandaa hafla ya kufunga, ambapo iliwasilisha ripoti ya shughuli za hisani ya Sheikha Hind Bint Maktoum na shughuli za Qur'ani ilionyeshwa.

Aidha Ahmed al-Zahed, mjumbe wa kamati ya maandalizi na msemaji wa mashindano hayo, katika hotuba yake alilitaja tukio hilo la Qur'ani kuwa mojawapo ya mashindano makuu ya Qur'ani kwa wanaume na wanawake na wakazi wa Imarati ambao ni wahifadhi wa Qur'ani.

Amebainisha kuwa, Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai (DIHQA) huandaa mashindano hayo kwa kushirikisha wahifadhi kutoka taasisi za Qur'ani kote katika nchi hiyo ya Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi.

Madhumuni ya mashindano hayo ni kustawisha harakati za kuhifadhi Qur’ani Tukufu na kuwaenzi wahifadhi Qur'ani na pia kuwatayarisha washindani wakuu kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani, alisema.

Pia hafla hiyo imehutubiwa ni Sheikh Ibrahim al-Mansouri, mkuu wa jopo la waamuzi, ambaye alisifu kiwango cha juu cha mashindano hayo.

Amesema moja ya matokeo yenye matunda ya kuandaa hafla hiyo ya Qur'ani ni kuenea kwa vituo vya kuhifadhi Qur'ani katika Imarati.

Wahifadhi 40 wa kiume na wahifadhi 51 wa kike walishindana katika sehemu mbili tofauti katika toleo hili la shindano, ambalo lilikuwa na kategoria kadhaa za kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

 

4195877

Habari zinazohusiana
captcha