IQNA

Binti Muirani ajibu maswali vizuri katika mashindano ya Qur'ani Dubai+PICHA

10:42 - November 10, 2016
Habari ID: 3470665
IQNA-Binti Muirani mwenye umri wa miaka tisa amejibu vizuri maswali ya jopo la majaji katika mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur’ani ya wanawake.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, siku ya Jumatano Hannaneh Khalfi ambaye ni mshiriki mwenye umri wa chini zaidi katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Sheikha Fatima Bint Mubarak alijibu maswali ya majaji katika vikao viwili vya mashindano.

Hannaneh alijibu maswali matatu ya Qur'ani kutoka kwa jaji Mmisriwakati wa asubuhi na aliweza kujibu maswali yote bila kufanya kosa lollote. Alhamisi ya leo Alasiri Hannaneh pia atapanda jukwaa na kujibu maswali ya majaji. Washiri wengine siku ya Jumatano walikuwa kutoka Mauritania, Bahrain, Iraq, Uturuki, Serbia na Sierra Leone.

Duru ya Kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Sheikha Fatima Bint Mubarak yameanza Novemba 6 na yataendelea hadi 18 mjini Dubai. Kuna washiriki 70 wa kike waliohifadhi Qur’ani kutoka nchi 72 za Kiarabu, Afrika, Amerika ya Latini, Asia na Ulaya ambao watashiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi Qur’ani maalumu kwa wanawake.

Washiriki ni kutoka umri wa miaka 9 hadi 23 ambapo washindi wa nafasi za kwanza, pili na tatu watapata zawadi za fedha taslimu AED 250,000; AED 200,000; na AED 150,000 kwa taratibu.

Mashindano hayo ni sehemu ya mashindano ya Qur’ani yajulikanayo kama Zwadi ya Kimatiafa ya Qur’ani Tukufu ya Dubai ambayo hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Binti Muirani ajibu maswali vizuri katika mashindano ya Qur'ani Dubai+PICHABinti Muirani ajibu maswali vizuri katika mashindano ya Qur'ani Dubai+PICHABinti Muirani ajibu maswali vizuri katika mashindano ya Qur'ani Dubai+PICHABinti Muirani ajibu maswali vizuri katika mashindano ya Qur'ani Dubai+PICHA

3544735.

captcha