Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu, katika mkutano huo, Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, amewasilisha ripoti kuhusu matukio ya hivi karibuni huko Ghaza na jinai za utawala wa Kizayuni katika eneo hilo la Palestina linalozingirwa, pamoja na matukio ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia kwa mara nyingine tena ameshukuru subira na ustahimilivu wa wananchi wenye msimamo thabiti wa Ghaza. Hali kadhalika amebainisha masikitiko yake makubwa kutokana na jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa uungaji mkono wa moja kwa moja wa Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi. Ayatullah Khamenei aidha amesisitiza kuhusu sera ya kudumu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuunga mkono vikosi vya muqawama au mapambano ya Kiislamu vya Palestina katika makabiliano na Wazayuni wanaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
Ayatullah Khamenei pia amesisitiza pia ulazima wa kuchukuliwa hatua madhubuti na nchi za Kiislamu pamoja na asasi za kimataifa kwa ajili ya kuunga mkono kwa pande zote na kwa vitendo watu wa Ghaza.
/3485892