IQNA

Mkutano baina ya viongozi wa Hizbullah na Hamas

21:12 - September 07, 2020
Habari ID: 3473144
TEHRAN (IQNA) - Ismail HaniYa, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameonana ana kwa ana na Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon na kuzungumza naye mambo muhimu yanayohusiana na kambi ya muqawama.

Mazungumzo ya ana kwa ana ya Jumapili baina ya Ismail Hania na Sayyid Hassan Nasrallah si mazungumzo ya kawaida, bali yana umuhimu mkubwa katika chanjaa zake zote. Mazungumzo hayo ni ya viongozi wawili wakuu wa kambi ya muqawama ambao wana imani thabiti, ya kiroho na kiitikadi na njia ya muqawama ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni na hawana matumaini kabisa na kufanikiwa mazungumzo ya mapatano baina ya baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel. Katika upande wa wakati huu wa kufanyika mazungumzo hayo, pia kuna umuhimu mkubwa, kwani sasa hivi tena, njama na uadui wa kambi ya Magharibi/Kiarabu/Kizayuni  dhidi ya kambi ya muqawama unadhihirishwa waziwazi bila ya kificho. 

Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS nchini Lebanon na mazungumzo aliyofanya na watu mbalimbali muhimu hasa baina yake na Sayyid Hassan Nasrullah, ni onyo kubwa kwa wale watawala wa nchi za Kiarabu ambao wanajidhalilisha mbele ya Wazayuni na Wamagharibi na ni sawa na kutangaza rasmi kwamba njama zozote dhidi ya kambi ya muqawama zitakabiliwa kwa nguvu zote na kwa umoja na mshikamano wa kambi hiyo nzima bila ya kujali umbali wa masafa ya kijiografia uliopo baina ya harakati na harakati nyingine ya muqawama.

3921130/

captcha