IQNA

Uislamu na Ukristo

Qari wa Iraq asoma aya katika Sura Al Imran kwa mnasaba wa Krismasi (+Video)

13:42 - December 28, 2022
Habari ID: 3476322
TEHRAN (IQNA) – Katika mnasaba wa Krismasi, ambayo ni siku ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa Nabii Isa Masih bin Maryam-Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake-,, qari wa Iraq alisoma aya za Sura Al Imran ya Qur’ani Tukufu.

Bibi Maryam, mama yake Nabii Isa au Yesu ametajwa katika Qur'ani Tukufu kuwa ni mwanamke mwema, ambaye hakuwa mtume bali alilelewa kama mtume na ambaye mwenendo wake ulikuwa kama ule wa mitume wa Mwenyezi Mungu.

Qari wa Iraq, Hassan al-Zabhawi, alisoma aya ya 37 ya Sura Al Imran, ambayo inazungumzia kuhusu riziki ya Mwenyezi Mungu aliyopelekewa Bibi Maryam.

"Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake. Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu."

captcha