IQNA

Pakistan yaunga mkono msimamo wa Canada wa kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu

15:25 - January 30, 2022
Habari ID: 3474868
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan amempongeza mwenzake wa Canada kutokana na hatua yake ya kulaani chuki dhidi ya Uislamu yaani Islamophobia huku akitaka kuwepo jitihada maalumu za kukabiliana na tatizo hilo.

Katika ujumbe kupitia ukuasa wake wa Twitter Jumapili, Imran Khan amempongeza Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau kutokana na mpango wake wa kumteua mwakilishi maalumu wa kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu.

Huku akimpongeza Trudeau kufuatia hatua yake hiyo, Imran Khan amesema: "Amechukua hatua wakati muafaka na  hilo ni jambo ambalo nimekuwa nikiomba lifanyike kwa muda mrefu."

Amesisitiza kuhusu haja ya kuwepo jitihada za kimataifa za kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu.

Siku ya Jumamosi Trudeau alitangaza kuwa chuki dhidi ya Uislamu ni jambo lisilokubalika na ameapa kuwa atahakikisha Canada ni nchi salama kwa Waislamu. Aidha amesema katika mpango wake wa kuangamia chuki dhidi ya Uislamu atateua mjumbe maalumu wa kukabiliana na tatizo hilo.

Mwaka jana serikali ya Canada ilitangaza Januaria 29 kuwa Siku ya Kitaufa ya Kukumbuka Hujuma dhidi ya Msikiti wa Quebec ambayo pia ni Siku ya Kukabiliana na Chuki Dhidi ya Uislamu.

Kwa mnasaba wa siku hii mwaka huu, serikali ya Canada imetoa taarifa na kusema inasimama pamoja na Waislamu nchini humo katika kukabiliana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Uislamu ni dini inayoenea kwa kasi zaidi Canada ambapo Waislamu wameongezeka kwa asilimia 82 katika kipindi cha muoongo moja uliopita. Hivi sasa Waislamu ni karibu asilimia 3.5 ya watu wote milioni 38 nchini Canada.

Disemba mwaka 2017, Trudeau katika ujumbe wake kwa Kongamano la Kuhuisha Uislamu alisema Waislamu nchini Canada wamekuwa na mchango mkubwa na ni rasilimali muhimu kwa nchi.

"Canada ina bahati kuwa na jamii ya Waislamu wenye harakati," alisema Trudeau katika ujumbe wake maalumu kwa njia ya video.

"Kwa muda wa miaka mingi, Waislamu nchini Canada wameweza kupata ustawi na kutoa mchango mkubwa kwa jamii  huku wakiwa wanadumisha ufungamano muhimu na nchi zao za asili na jambo hilo limewawezesha kuwa na turathi nzuri ya utamaduni.

3477602

captcha