IQNA

Nasrallah: Uchaguzi wa rais Marekani umeweka wazi sura halisi ya utawala huo wa kibeberu

13:18 - November 12, 2020
Habari ID: 3473353
TEHRAN (IQNA) -Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala wa rais anayeondoka wa Marekani, Donald Trump ndiyo serikali mbaya zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Sayyid Hassan Nasrallah amesema hayo katika hotuba aliyoitoa jana Jumatano kwa mnasaba wa Siku ya Mashahidi wa Hizbullah na kuongeza kuwa, uchaguzi wa hivi karibuni wa Marekani umefichua sura halisi ya nchi hiyo ya kibeberu.

Amesema: Nawaomba wanaoipigia debe demokrasia ya Marekani waangalie mfano huu na watueleze iwapo tuifuate (US) au la. Tazama hali ya maisha katika miji mikubwa ya Marekani, watu wanavyoishi katika mahema bila usalama wa kijamii, kesi za kupindukia za Covid-19, magonjwa ya kisaikolojia, uraibu (wa mihadarati), idadi kubwa ya watu magerezani, na ubaguzi usio na kifani."

Sayyid Nasrallah amekumbusha kuwa, sera kuu ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi ni kutanguliza mbele maslai ya utawala haramu wa Israel, iwe ni serikali ya Republican au Democratic, sera hiyo ni madhubuti haiwezi ikabadilika. 

Ameeleza bayana kuwa, "haijalishi ni rais yupi yuko madarakani Marekani, wote hukimbilia kuuimarisha utawala wa Kizayuni. Kwetu sisi hatuoni tofauti yoyote."

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amebainisha kuwa, harakati hiyo ya muqawama itaendelea kupambana na genge la kigaidi la Daesh (ISIS) katika nchi za Syria na Iraq, ili kulifanya lisipanue satua yake katika nchi nyingine za eneo la Asia Magharibi.

Ameongeza kuwa, maafisa wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani wana wasi wasi mkubwa baada ya Trump kumfuta kazi Mkuu wa Pentagon, Mark Esper na kueleza kwamba, yumkini anapanga kutekeleza njama ndani na nje ya Marekani katika kipindi hiki kilichosalia cha uongozi wake.

3934730/

captcha