IQNA

Msomi wa Misri

Watoto wapewe mafunzo sahihi ya Qur'ani kuepusha misimamo mikali

12:36 - July 12, 2017
Habari ID: 3471063
TEHRAN (IQNA)-Mtaalamu wa masuala ya kidini nchini Misri amesema watoto wanapaswa kuepwa mafunzo sahihi ya Qur'ani ili kunusuru vizazi vijavyo visitumbukie katika misimamo mikali na utumiaji mabavu.

Sayyed Musaad, Naibu Mkuu wa Idara ya Waqfu mjini Cairo ameyasema hayo Jumanne wakati wa kuwattunuku zawadi washindi wa mashindano ya Qur'ani.

Mashindano hayo yaliandaliwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya waliohifadhi Qur'ani kaitka taasisi za Qur'ani zisizo za kiserikali.

Aliongeza kuwa, wazazi wanapaswa kujitahidi kuwapa watoto wao mafunzo sahihi ya Qur'ani Tukufu ili kuwawezesha kujizuia kutumbukia katika misimamo mikali na utumiaji mabavu.

Sayyed Musaad amesisitiza kuwa, Qur'ani Tukufu inamfunza mwanadamu namna ya kuishi kwa kutafakari kuhusu mafundisho ya kitabu hicho kitukufu lengo likiwa ni kuletta usalama na amani katika jamii.

Kila mwaka katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani jamii za Waislamu kote duniani huandaa mashindano ya Qur'ani Tukufu.

3618163

captcha