IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya wanachuo wa vyuo vikuu vya kidini Iran

15:18 - November 24, 2016
Habari ID: 3470695
IQNA-Mashindano ya kimatiafa ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya wanafunzo wa vyuo vikuu vya Kiislamu (Hawza) nchini Iran yamepangwa kufanyika katika mji mtakatifu wa Qum.

Akizungumza na IQNA, mkuu wa vyuo vya Kiislamu nchini Iran Hujjatul Islam Mustafa Razavi amesema mashindano hayo yataandaliwa kwa pamoja na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustada SAW kwa himaya ya Shirika la Waqfu na Misaada Iran.

Ameongeza kuwa, mji mtakatifu wa Qum utakuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya Qur'ani mnamo Mei 2017 sambamba na Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yatakayofanyika katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika mashindano hayo wanafunzi Wairani katika vyuo vikuu vya kidini watashindana na wenzao kutoka nchi zingine 100.

Kategoria za mashindano ni pamoja na qiraa ya Qur'ani Tukufu, kuhifadhi Qur'ani Tukufu na pia Makala za utafiti kuhusu Qur'ani Tukufu na ustaarabu wa Kiislamu.


3461505
captcha