IQNA

Mashindano ya Qurani ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cairo

8:19 - November 08, 2016
Habari ID: 3470662
Mashindano ya Qur'ani ya wanafunzi kwa ajili ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cairo yameanza.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo ambayo pia yatajumuisha maswali kuhusu utamaduni wa Kiislamu yameandaliwa na Idara ya Utamaduni ya Kitengo cha Vijana katika Chuo Kikuu cha Cairo.

Mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani yaliyoanza Jumapili yanawajumuisha wanachuo vya vitivo kadhaa vya Chuo Kikuu cha Cairo.

Katika masindano hayo yatakayoendelea kwa muda wa siku tano wanafunzi watashindana katika kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, kuhifadhi Juzuu 20,15,10 na 15 kwa kuzingatia misingi ya tajweed.

Chuo Kikuu cha Cairo ni chuo kikuu muhimu zaidi cha umma nchini humo na ni cha pili kuanzishwa nchini humo baada ya kile cha Kiislamu cha Al Azhar.

3543841

captcha