IQNA

Jinai za Israel

Kauli ya kiongozi wa Hamas baada ya Israel kuwaua shahidi watoto na wajukuu wake

10:33 - April 11, 2024
Habari ID: 3478669
IQNA-Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, Hamas, amethibitisha habari ya kuuawa shahidi watoto na wajukuu zake katika shambulio la kinyama la utawala wa Kizayuni na akasema: "kwa machungu haya na kwa damu hii tunajenga matumaini, mustakbali na uhuru wa watu wetu, piganio letu na taifa letu".
Jeshi katili la utawala wa Kizayuni jana liliilenga gari iliyokuwa imewabeba watoto na wajukuu wa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, na kutokana na jinai hiyo watu saba wa familia ya Ismail Haniya waliuawa shahidi.
 
Watoto watatu wa kiume wa Haniya waliouawa shahidi katika shambulio hilo wametambulika kuwa ni Hazem, Amir na Muhammad.
Watoto na wajukuu hao wa Kiongozi wa Hamas walikuwa wameelekea kambi ya wakimbizi Wapalestina ya Al-Shati kwenda kuwasalimia na kuwatakia Idi njema wakazi wa kambii hiyo kwa mnasaba wa Sikuu ya Idul-Fitri iliyosherehekewa jana. 
 
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas amesema: "Ninamshukuru Allah kwa heshima hii aliyotupa ya kufa shahidi wanangu watatu na wajukuu zangu".
Ismail Haniya: Ninamshukuru Allah kwa heshima hii aliyotupa ya kufa shahidi wanangu watatu na wajukuu zangu

Katika taarifa aliyotoa kupitia televisheni, Haniya amesisitiza kwa kusema: "wakaliaji ardhi kwa mabavu wanadhani kwamba kwa kuwalenga watoto wa viongozi, watavunja azma ya watu wetu, lakini umwagaji damu huu utaimarisha tu uthabiti wetu katika misingi yetu na kushikamana kwetu na ardhi yetu."

Kiongozi wa Hamas ameongezea kwa kusema: “wanangu walibaki Ghaza na hawakuondoka katika eneo hilo; kama ilivyo kwa watoto wote, watu wetu wanalipa gharama kubwa katika damu ya watoto wao, na mimi ni mmoja wao.”

Haniya ameuhutubu utawala wa Kizayuni kwa msisitizo akisema: "tunaiambia Israel: kile ambacho hamjaweza kukipata kwa kufanya uharibifu, mauaji ya halaiki na uangamizaji, hamtakipata kwenye meza ya mazungumzo".

 
captcha