IQNA

Harakati za Qur'ani

Haram ya Hadhrat Abbas yaandaa kikao cha Qur’ani nchini Senegal

18:02 - April 10, 2024
Habari ID: 3478664
IQNA –Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas (AS) nchini Iraq imeandaa mkusanyiko wa qiraa ya Qur'ani Tukufu nchini Senegal kuadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kama ilivyoripotiwa na Al-Kafeel, programu hiyo ilikuwa ni mkusanyiko wa usomaji na Sala na Qur’ani Tukufu uliofanyika Dakar, mji mkuu wa Senegal, chini ya uangalizi wa idara hiyo.

Katika mkutano huu wa kiroho, Sheikh Mustafa Diba alitoa hotuba akisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja kwa amani miongoni mwa makundi mbalimbali ya kijamii.

Aliwataka hadhirina kukuza moyo wa upendo na umoja, unaolenga kukuza jamii iliyojaa urafiki na mapenzi.

Kituo cha Masomo ya Kiafrika, kinachohusishwa na Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas (AS), hutuma wahubiri katika nchi mbalimbali za Afrika. Dhamira yao ni kuelimisha watu kuhusu kanuni na mafundisho ya Uislamu na kutekeleza mipango ya kielimu na ya kibinadamu.

 

4209578

captcha