IQNA

Ripoti

Mke wa kinara wa Daesh (ISIS) afichua siri kubwa gaidi al Baghdadi

14:36 - February 17, 2024
Habari ID: 3478367
IQNA-Wakuu wa mahakama nchini Iraq wametangaza kuwa familia ya Abu Bakar al-Baghdadi, kinara wa zamani wa genge la kigaidi la Daesh (ISIS) imesailiwa baada ya kurejeshwa Iraq kutoka nje ya nchi.

Baraza la Mahakama la Iraq limetoa taarifa na kusema: Familia ya Al-Baghdadi imekamatwa na kurudishwa Iraq na taarifa zao zimesajiliwa na kurekodiwa chini ya uangalizi wa moja kwa moja wa jaji mwenye mamlaka katika Mahakama ya Kwanza ya Upelelezi ya Karkh. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, uchunguzi wa kufichua siri muhimu zaidi za genge la kigaidi la Daesh (ISIS) unaendelea.

Mwezi Novemba 2019, serikali ya Uturuki ilitangaza habari ya kukamatwa mjane wa al-Baghdadi pamoja na watu wengine 10, akiwemo binti yake.

Afisa wa Uturuki alisema mjane huyo alikuwa "mke wa kwanza" wa al-Baghdadi na alikamatwa mwezi Juni 2018 katika mkoa wa Hatay wa Uturuki, kwenye mpaka wa Syria.

Kwa mujibu wa afisa huyo wa serikali ya Uturuki, mke huyo wa kwanza wa kiongozi wa zamani wa magaidi wa Daesh ametoa taarifa nyingi kuhusu mumewe na mambo ya ndani ya genge la ISIS. Wakati huo, vyombo vya habari vya Uturuki viliripoti kwamba jina la mke huyo wa kwanza wa al Baghdadi ni Asma Fawzi Mohammad al Qubaysi na jina la bintiye ni Leila.

Katika maohiano Asma amesema, Abu Bakr al-Baghdadi alitaka kupanua ukhalifa wake hadi Rome. Aidha ameongeza kuwa: "Sikuwahi kumuona  al-Baghdadi alihuzunishwa na kifo cha wenzake.

Pia alisema: Abu Bakr al-Baghdadi alipenda  sana anasa na wanawake, na kwa sababu hiyo, aliugeuza ukhalifa wa Kiislamu kuwa ukhalifa wa wanawake. Alikuwa na masuria 10. Alikuwa na wake watatu na masuria 10 zaidi yangu. Mmoja wa wake zake alikuwa Msiria na mwingine alikuwa Mkekeni.

Kwa upande wake, tovuti ya Al Arabiya imeripoti kuwa, mke huyo wa al Baghdadi amefichua taarifa muhimu kuhusu mumewe huyo ikiwa ni pamoja na kwamba alikuwa na wake wanne na masuria 10 kama ambavyo amefichua pia kwamba watu waliokuwa wanafuatana na al Baghdadi walikuwa na hisia kali za kufanya ngono na wanawake kiasi kwamba ameiita dola yao kuwa ni khilafa ya wanawake si khilafa ya Kiislamu.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, Umoja wa Mataifa unatabiri kwamba, muundo jumla ya genge la Daesh hivi sasa una magaidi baina ya 5000 hadi 7000 na wamejificha katika maeneo tofauti ya Iraq na Syria.

4200106

captcha