Tukio hilo limesababisha kuongezeka kwa doria katika eneo hilo huku mamlaka ikitafuta mshukiwa sambamba na kubaini lengo lake.
Mkuu wa polisi Oscar Perez alisema kuwa ufyatuaji risasi ulifanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Rhode Island.
Shambulio hilo linakuja huku kukiwa na hali ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu nchini Marekani kufuatia vita kati ya Wapalestina na utawala wa Israel.
Mwathiriwa, ambaye ni huswali katika msikiti huo, alikuwa katika meza ya kuuza "bidhaa za Kiislamu" alipopigwa risasi sehemu ya chini ya mwili wake.
Afisa aliyekuwa karibu alisikia milio ya risasi na akaelekea eneo la tukio mara moja. Mwathiriwa mwenye umri wa miaka 52 baadaye alisafirishwa hadi hospitali kwa matibabu ya majeraha yasiyo ya kutishia maisha.
Katika mahojiano na WPRI, Perez alielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo na kusisitiza kuwa polisi watakuwa wakilinda usalama katika eneo hilo ili kuhakikisha usalama wa kila mtu.