IQNA

Alireza Bijani akisoma aya za Surah Al Furqan

TEHRAN (IQNA) – Qari wa kimataifa wa Iran Alireza Bijani hivi karibuni amesoma aya za 63 hadi 71 za Surah Al-Furqan katika Qur'ani Tukufu.
Usomaji wa Aya za Alireza Bijani kutoka katika Surah Al-Furqan

Hapa chini ni tarjama ya aya hizo:

  1. Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama! 

 

  1. Na wale wanao kesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama. 

 

  1. Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi. 

 

  1. Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya. 

 

  1. Na wale ambao wanapo tumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo. 

 

  1. Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara, 

 

  1. Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka. 

 

  1. Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 

 

  1. Na aliye tubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kweli kweli kwa Mwenyezi Mungu. 
Kishikizo: qurani tukufu ، qari ، iran