IQNA

Qari Anvari wa Iran, Ustadh Amir Hossein Anvari akisoma aya katika Sura Al-Anaam

TEHRAN (IQNA) – Amir Hossein Anvari, qari kijana wa Kiirani, akisoma aya katika Surah Al-Anaam ya Qur’ani Tukufu mwezi uliopita.

Usomaji  huo ulifanyika wakati wa mafunzo yaliyofanyika kwa ajili ya kuboresha ujuzi wa maqari vijana wakuu nchini.

Alisoma  tafsiri ya aya ya 12-21

Sema; ‘Ni vya nani viliomo mbinguni na ardhini?’ Sema; ‘Ni vya Mwenyezi Mungu, Amejiandikia rehema, na atakukusanyeni Siku ya Kiyama isiyo na shaka ndani yake, Wale ambao wamezitia khasarani nafsi zao, hawaamini.

Ni vyake vyote vinavyotulia usiku na mchana, Yeye ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Sema; Je? nimfanye yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu kuwa mlinzi? Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi, Analisha wala halishwi, Sema; Nimeamrishwa niwe wa kwanza kunyenyekea kwake. Usiwe miongoni mwa washirikina.

Sema; Hakika mimi naogopa nikimuasi Mola wangu Mlezi adhabu ya Siku ya Qiyama.

Atakayeepushwa siku hiyo atamrehemu, huko ni ushindi ulio wazi.

Mwenyezi Mungu akikufikieni kwa dhiki, hapana wa kukuondosheeni isipokuwa Yeye.,na akikugusisha kwa kheri, basi Yeye ni Muweza wa kila kitu.

Yeye ndiye Mshindi juu ya waja wake, Yeye ndiye Mwenye hekima, Mwenye khabari.

Sema; ‘Ni kitu gani kilicho kikubwa katika ushahidi?  Sema; ‘Mwenyezi Mungu ni shahidi baina yangu na nyinyi, Nimeteremshiwa Qur'ani hii ili nikuonye wewe na kila inayowafikia,Je, mnashuhudia kwamba wapo miungu badala ya Mwenyezi Mungu? Sema; ‘Mimi sishuhudii, Sema; Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja tu, na mimi nimejitenga na hao mnaowashirikisha.

Wale tulio wapa Kitabu wanamjua Mtume Muhammad kama wanavyowajua watoto wao, Lakini wale ambao wamezitia hasarani nafsi zao hawaamini.

Ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo au anaye zikadhibisha Aya zake? Madhalimu hawatafanikiwa kamwe.

 

 
 

3485462



Kishikizo: qari ، qurani ، kusoma qurani