IQNA

Utakatifu wa Qur'ani

Rais wa Urusi asema Qur'ani ni Takatifu kwa Waislamu, inapaswa kuwa Takatifu kwa wengine

11:54 - July 01, 2023
Habari ID: 3477219
Rais wa Urusi (Russia) Vladimir Putin alisema Qur'ani ni takatifu kwa Waislamu na inapaswa kuwa takatifu kwa wengine pia.

Rais wa Urusi (Russia) Vladimir Putin alisema Qur'ani ni takatifu kwa Waislamu na inapaswa kuwa takatifu kwa wengine pia.

Akizungumza katika ziara yake huko Derbent katika Jamhuri ya Dagestan inayojiendesha ya Shirikisho la Urusi siku ya Jumatano, aliongeza kuwa, kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu sio jinai katika baadhi ya nchi bali ni jinai ambayo anayeitenda  nchini Russia ataadhibiwa.

"Katika nchi yetu, huu ni uhalifu kwa mujibu wa Katiba na kanuni ya adhabu," alisema.

"Siku zote tutafuata sheria hizi."

Putin alitembelea msikiti wa kihistoria wa Derbent na kukutana na wawakilishi wa Waislamu kutoka Dagestan.

Kiongozi huyo wa Urusi alipewa zawadi ya nakala ya Qur'ani, kitabu kitakatifu cha Waislamu, walipokuwa wakisherehekea sikukuu ya Eid-al-Adha.

Aliwashukuru wawakilishi kwa zawadi hiyo.

3484136

captcha