IQNA

Haki za Waislamu

Gambia: Wanafunzi Waislamu washtaki shule kwa marufuku ya Hijab

8:13 - May 11, 2023
Habari ID: 3476987
TEHRAN (IQNA) – Mamia ya wanafunzi wa kike wa Kiislamu wamezishtaki shule kadhaa nchini Gambia, wakizituhumu kwa kupiga marufuku vazi lao la Hijabu.

Umati wa wanafunzi waliovalia Hijabu wafuasi wao walikusanyika katika mahakama kuu ya Banjul kushtaki shule tano kwa madai ya kuwazuia kuvalia vifuniko shuleni.

Wanafunzi hao walidai kuwa vitendo vya shule zao viliwasababishia mfadhaiko wa kihisia na aibu na kukiuka haki zao za kimsingi za binadamu na utu wao. Wanataka walipwe zaidi ya dola laki tatu kama fidia.

Pia wanazitaka mamlaka kupitisha sheria inayowaruhusu kuvaa Hijabu shuleni.

Shule hizo zilikanusha kukika sheria katika nyaraka zilizowasilishwa mahakamani.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 20, 2023 na Jaji Jaiteh wa mahakama kuu ya Banjul kwa ajili ya kusikilizwa na kutolewa hukumu.

Baadhi ya shule katika kesi hiyo ni za Kikristo lakini wanafunzi wao wengi ni Waislamu.

Gambia ni nchi yenye Waislamu wengi na Wakristo wachache.

3483514

Kishikizo: gambia waislamu hijabu
captcha