IQNA

Diplomasia

Rais Raisi: Utawala wa Kizayuni umekasirishwa na hatua ya kuhuishwa uhusiano kati ya Iran na Saudia

21:19 - May 03, 2023
Habari ID: 3476951
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Iran ameashiria kukasirishwa utawala wa Kizayuni kufuatia kuhuishwa uhusiano kati ya Iran na Saudia na akasema: Maadui khususan utawala wa Israel wamekasirishwa na hatua hii na sababu yake ni njama wanazofanya za kueneza migawanyiko.

Akizungumza katika mahojiano na  televisheni ya al Mayadeen ya Lebanon,  Rais wa Iran ameongeza kuwa: Iran na Saudi Arabia ni nchi mbili zenye taathira katika eneo la Mashariki ya Kati na uhusiano wa pande mbili utakuwa na manufaa mengi.

Aidha amesema  amesema: Hali ya mambo hivi sasa imebadilika na kwamba utawala wa Kizayuni hauwezi kujidhaminia usalama ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.

ais Sayyid Ebrahim Raisi ameashiria matatizo ya ndani yanayouzonga utawala wa Kizayuni na kuongeza kuwa:Mikataba kama ule wa Sharam- Sheikh, wa Oslo na Camp David haiwezi kuudhaminia utawala huo usalama. Amesema,leo hii uamuzi uko mikononi mwa mujahidina wa Kipalestina na si katika meza ya mazungumzo ya kisiasa.   

Rais wa Iran amegusia pia kuhusu uwezo wa kijeshi na kiulinzi wa nchi hii na kusema: Katika upande wa uwezo wa kijeshi na kiulinzi si tu Iran imeweza kujitegemea bali ni kati ya nchi zilizopiga hatua katika sekta ya ulinzi duniani. Raisi amesisitiza kuwa: Katika miaka 44 iliyopita adui hajafanya uinga wowote dhidi ya Iran si kwa sababu hakutaka bali ni sababu hana ubavu wa kufanya hivyo. 

Katika sehemu nyingine ya matamshi yake, Rais Ebrahim Raisi ameashiria kujiunga Iran na Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai na  kueleza kuwa: Hatua hiyo imeisaidia Iran kuandaa mazingira ya kushirikiana na miundomsingi ya Asia na pia tuko tayari kujiunga na kundi la BRICS. 

/3483419

captcha