IQNA

Uislamu nchini Ufilipino

Ufilipino Inaitangaza Februari 1 kuwa Siku ya Kitaifa ya Hijabu

13:31 - November 17, 2022
Habari ID: 3476101
TEHRAN (IQNA) – Bunge nchini Ufilipino limepitishwa sheria ya kuitangaza Februari 1 kila mwaka kuwa Siku ya Kitaifa ya Hijabu ili kuongeza ufahamu wa desturi za Waislamu.

Sheria hiyo imepitishwa baada ya kuidhinishwa na wabunge 274 walioshiriki katika kikao hicho cha Jumanne.

Muswada wa sheria hiyo ulitayarishwa na Mwakilishi wa Maguindanao. Bai Dimple Mastura, Mwakilishi wa Basilan Mujiv Hataman, Mwakilishi wa Wilaya ya 1 ya Lanao del NorteMohamad Khalid Dimaporo na wabunge wengine. Lengo la sheria hiyo limetajwa kuwa ni kuhimiza wanawake kuvaa hijabu, kukomesha ubaguzi wa Waislamu wanaovaa Hijabi na kwa ujumla kuondoa dhana potofu kuhusu dini tukufu ya Kiislamu.

“Serikali inatambua nafasi ya wanawake katika ujenzi wa taifa na itahakikisha usawa wa kimsingi wa wanawake na wanaume mbele ya sheria. Utekelezaji huru wa ibada ya kidini, bila ubaguzi na au upendeleo, vitaruhusiwa milele," maelezo ya muswada huo yalisema.

"Siku ya Hijabu ya Kitaifa itaadhimishwa kila siku ya kwanza ya Februari ili kuonyesha haki za hijabu na mila ya Waislamu ya kuvaa hijabu. Wanawake wa Kiislamu na wasio Waislamu watahimizwa kuvaa hijabu siku hii,” iliongeza.

Kwa mujibu wa mswada huo, "hijabu" inarejelea "pazia linalofunika kichwa na kifua, ambalo huvaliwa haswa na mwanamke wa Kiislamu aliyepita umri wa balehe mbele ya wanaume watu wazima nje ya familia zao." Neno hilo pia hutumiwa kufafanua vazi lolote la kichwa, uso, au mwili linalovaliwa na wanawake Waislamu “ambalo linapatana na kiwango fulani cha staha.”

Hijabi, kwa upande mwingine, ni mwanamke wa Kiislamu aliyevaa Hijabu. "Taasisi za serikali, shule na sekta binafsi zitahimizwa kuadhimisha tukio hili kwa namna ambayo itakuza uelewa na ufahamu miongoni mwa wafanyakazi wake na wanafunzi wa lengo la kampeni," ilisema hatua hiyo.

Hatua hiyo pia inaidhinisha Tume ya Kitaifa ya Waislamu  Wafilipino kama wakala unaoongoza katika kukuza na kuongeza fahamu kuhusu kuvaa hijabu.

"Tume hii itafanya shughuli ambazo zitalenga kuongeza uelewa wa hijab kama chaguo la maisha miongoni mwa wanawake wa Kiislamu. Kwa maana hii, inaweza kufanya mikutano, kampeni za usambazaji wa habari na misukumo mingine ya elimu ili kufikia malengo ya Sheria hii kwa ufanisi,” iliongeza.

3481281

captcha