IQNA

Mkenya, Watanzania ni miongoni mwa washindi Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran

21:45 - March 05, 2022
Habari ID: 3475011
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran yamemalizika Jumamosi jioni mjini Tehran huku miongoni mwa washindi wakiwa ni wawakilishi wa Kenya na Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa katika Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur’ani kitengo cha kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu, nafasi ya kwanza imechukuliwa na Hissan Muhammad Bakour wa Syria, huku Mohammad Rafaat Albana wa Indonesia akishika nafasi ya Indonesia naye Ustadh Haitham Sagar Ahmad  wa Kenya ameshika nafasi ya tatu. Katika shindano la wanawake la kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu, nafasi ya kwanza imeshukwa na Tahira Naibu wa Iran huku Zahra Abduljabar akiwa wa pili naye Ashura Amani wa Tanzania amechukua nafasi ya tatu. Aidha katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu shindano la washichana wa shule nafasi ya kwanza imeshikwa na Zahra Khalili  wa Iran huku Asma Saleh wa Tanzania akishika nafasi ya pili nayo nafasi ya tatu imechukuliwa na Humaira Kunec wa Uturuki.

Katika kitengo cha Qiraa Tahqiq nafasi ya kwanza imemuendea Muwahid Amin wa Iran naye Thamaruddin  Samadof wa Tajikistan ameshika nafasi ya pili huku Oweys Ahmadian wa Afghanistan akiwa wa tatu. Halikadhalika  katika Qiraa Tartila Sayyid Hujjat Tarhami ameshika nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikiwa ni ya Hussein Ibrahim wa Misri na Mustafa Zahid wa Morocco ameibuka wa tatu.

Jumla ya makari 62 na wahifadhi Qur'ani kutoka nchi 29 wanashindana katika hatua hii ya hafla hiyo, ambayo inafanyika karibu.

Sambamba na mashindano ya kawaida ya 38 ya kimataifa ya Qur'ani tukufu, yamefanyika pia mashindano ya saba ya Qur'ani kwa wanafunzi wa skuli za nchi za Ulimwengu wa Kiislamu na vilevile mashindano ya tano ya Qur'ani katika Ulimwengu wa Kiislamu kwa washiriki wenye ulemavu wa macho na halikadhalika mashindano ya wanawake.

Kutokana na janga la corona, aghalabu ya walioshindana katika mashindano hayo wameshiriki kwa njia ya intaneti huku baadhi wakishiriki ana kwa ana katika ukumbi. Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran huandaliwa kila mwaka na Shirika la Wakfu na Masuala ya Kheri la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

4040487

Habari zinazohusiana
captcha