IQNA

Bintiye msemaji wa Rais wa Russia avutiwa na Uislamu, asema atafunga Ramadhani

12:38 - April 24, 2020
Habari ID: 3472697
TEHRAN (IQNA) – Elizaveta, bintiye msemaji wa Rais wa Russia Dmitry Peskov ametangaza kuwa atafunga saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika taarifa kupitia ukurasa wake wa Instagram, Elizaveta amesema tokea utotoni hajafuata dini yoyote lakini anasema huzingatia sana mafundisho ya kidini. Elizaveta amenukuliwa na tovuti ya http://islam.ru/ akisema kuwa, ingawa anajitambua kuwa mwenye imani ya kidini lakini hafuati Ukristo wa Kiothodoxi ambao unafuatwa na Wakrsito wa Russia. Anasema anasema amesoma kuhusu itikadi ya Kibudhha lakini pamoja na hayo fikra zake ziko karibu zaidi na Uislamu.

Elizaveta amesema ana mpango wa kufunga Saumu siku zote za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Baba yake Elizaveta, Dmitry Peskov amekuwa msemaji wa Rais Vladimir Putin wa Russia tokea mwaka 2012. Peskov aliwahi kuishi Pakistan wakati baba yake alikuwa balozi wa Shirikiso la Sovieti nchini humo. Peskov alihitimu masomo yake katika Kituo cha Masomo ya Nchi za Afrika na Asia katika Chuo Kikuu cha Moscow na mbali na lugha yake asili ya Kirussia, anazungumza pia Kiingereza, Kituruki na Kiarabu.  

3893753

captcha