IQNA

Uhaba wa wanawake wahubiri na wasomaji Qur'ani Misri

11:27 - January 25, 2018
Habari ID: 3471371
TEHRAN (IQNA)-Sheikh Khalid al Jundi, mwanachama wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu Misri amesikitishwa na uhaba wa wasomaji Qur'ani wanawake nchini humo.

Sheikh Jundi amesema idadi ya wahubiri na mubalighina wanawake wenye uwezo wa kuzungumza katika mihadhara na vituo vya kielimu Misri ni ndogo sana.

Aidha amesema pia kuna uhaba mkubwa wa wasomaji Qur'ani wanawake nchini Misri na kwa msingi huo ametaka kuwepo jitihada za kuhakikisha kuna idadi ya kutosha ya wanawake wenye uwezo wa kusoma Qur'ani katika mihadhara maalumu ya wanawake.

Sheikh al Jundi ametoa wito kwa Wamisri kurejea katika zama ambazo ilikuwa ni fahari kwa familia kuwa na qarii wa Qur'ani huku akisisitiza umuhimu wa malezi bora kupitia kuwafundisha watoto Qur'ani.

/3684565

captcha