IQNA

Amir wa Makka asema Wairani ni ndugu zetu wa kidini

11:05 - September 03, 2017
Habari ID: 3471153
TEHRAN (IQNA)-Mwanamfalme Khalid al Faisal ambaye ni amiri wa mji mtakatifu wa Makka amewataja Wairani kuwa ndugu wa kidini wa watu wa Saudi Arabia.

Al Faisal amenukuliwa akiyasema hayo hivi karibuni katika mkutano na waandishi habari ambapo alielezea matumaini yake kuwa Mahujaji Wairani watakamilisha Ibada ya Hija pasina kukumbwa na matatizo yoyote. Aidha amesema: "Mahujaji Wairani ni ndugu zetu wa kidini na tunawakaribisha kwa moyo mkunjufu."

Amir Al Faisal ameelezea matumaini yake kuwa Mahujaji Wairani wakirejea nyumbani watakuwa na kumbukumbu zuru za safari yao ya Ibada ya Hija nchini Saudi Arabia. Aidha amebainisha kuwa katika msimu wa Hija mwaka huu, Mahujaji Wairani hawajalbiliwa na tatizo lolote.

Aidha alibainisha kuwa, mwaka huu Mahujaji waliotoka nchi ya Saudia walikuwa ni 1,752,014 ikiwa ni ongezeko la 426,263 ikilinganishwa na mwaka jana.

Kwa mujibu wa Idara ya Hija Saudi Arabia, Indonesia ndio nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Mahujaji mwaka huu wa 1438 Hijria sawa na 2017 Miladia. Inatazamiwa kuwa Waindonesia 221,000 watatekeleza ibada ya Hija mwaka huu. Nchi zingine zenye idadi kubwa ya Mahujaji ni Pakistan (179,210), India (170,000), Bangladesh (128,000), Nigeria (95,000) na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (86,500).

3637046

captcha