Hukumu ya kesi ya mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu na kiongozi wa kimaanawi wa harakati ya kimapinduzi ya Wabahrain ilitarajiwa kutolewa jana Alhamisi lakini sasa imeahirishwa hadi tarehe 26 Septemba mwaka huu.
Utawala wa kiukoo wa Aal Khalifa unamtuhumu Sheikh Isa Qassim kwamba
anaeneza chuki za kimadhehebu miongoni mwa watu wa Bahrain. Mbali na
hayo utawala huo ulimvua uraia wa Bahrain Sheikh huyo hapo tarehe 20
mwezi Juni uliopita jambo ambalo liliamsha hasira kubwa ya wanachi wa
nchi hiyo na wa mataifa mengine huru duniani. Kufuatia hatua hiyo ya
kibaguzi ya utawala wa Bahrain, eneo la ad-Diraz lililoko magharibi mwa
mji mkuu wa Bahrain limebadilika na kuwa kituo cha mikusanyiko na
malalamiko ya kila siku ya Wabahrain dhidi ya ukamdamizaji na uonevu wa
utawala wa nchi hiyo dhidi ya mwanazuoni huyo mashuhuri wa Kishia.
Ni uungaji mkono huo mkubwa wa wananchi kwa kiongozi huyo mashuhuri na
matokeo hatari ya kuchukuliwa hatua ya kuhukumiwa kwake mahakamani ndiko
kumewatia hofu watawala dhalimu wa nchi hiyo na kuwafanya waakhirishe
kuhukumiwa kwake. Inaonekana kuwa kwa kuakhirisha mara kwa mara
kuhukumiwa mwanazuoni huyo, watawala wa Bahrain wanapima hisia na
uungaji mkono wa wananchi kwa kiongozi huyo wakidhani kuwa uungaji mkono
huo utapungua na hivyo kupata fursa nzuri ya kumukumu bila ya
kuhatarisha utawala wao wa mabavu nchii humo. Jambo linalosahaulika na
utawala wa Bahrain ni kuwa hautaweza kufikia malengo yake maovu kwa
kuwapokonya uraia na kuwafunga jela wanazuoni na wanafikra walio na
fikra kama za Sheikh Isa Qassim.
Utawala huo una wasiwasi mkubwa kwamba kwa kumuhukumu Sheikh Isa Qassim
huenda ukachochea zaidi hisia na uungaji mkono wa wananchi kwa kiongozi
huyo wa kidini na hivyo kutoweza kudhibiti hali ya mambo nchini na
wanamapinduzi wa nchi hiyo. Ni miezi mitatu sasa tokea eneo la ad-Diraz
anakoishi Sheikh Qassim limegeuka na kuwa eneo la makabaliano makali kati
ya wananachi wanamapinduzi na utawala dhalimu wa Manama. Licha ya
utawala huo kutumia mbinu za ukandamizaji na unyanyasaji dhidi ya
wanananchi lakini wanachi ndio wamekuwa washindi wa mwisho kufikia sasa
kwa kubuni njia tofauti za kukabiliana na ukandamizaji wa askari jeshi
wa utawala huo.
Bahrain imekuwa ikishuhudia maandamano ya amani ya wananchi dhidi ya
utawala wa Aal Khalifa tangu mwezi Februari mwaka 2011. Wananchi wa
Bahrain wanataka marekebisho ya kisiasa, uhuru, uadilifu, kukomeshwa
vitendo vya ubaguzi na kuingia madarakani serikali iliyochaguliwa kwa
njia ya kidemokrasia. Utawala wa Bahrain umewanyima wananchi wa nchi
hiyo haki zao zote.
3460943