IQNA

Waislamu Kenya wakasirishwa na marufuku ya Hijabu

23:17 - September 29, 2014
Habari ID: 1455483
Mahakama moja ya Kenya imetoa uamuzi wa kupiga marufuku vazi la Hijabu katika shule moja nchini humo jambo ambalo limewakasirisha sana Waislamu wakiwemo wazazi na wanazuoni wa Kiislamu ambao wameitaja hukumu hiyo kuwa ni hatua nyuma katika uhuru wa kuabudu nchini humo.

Mnamo Septemba 23, Mahakam ya Isiolo, mashariki mwa Kenya, ilitoa uamuzi wa kuwazuia wanafunzi wasichana Waislamu kuvaa  Hijabu wakiwa katika Shule ya Upili ya St Kiwanjani. Mahakama hiyo imedai kuwa ni kinyume cha sheria  za Kenya kwa wasichana kuvaa  vazi la Hijabu linalojumuisha mtandio  na suruali ndefu. Uamuzi huo wa kuzuia vazi la Hijabu umefuatia kesi iliyowasilishwa na Kanisa la Methodist la Kenya ambalo limedai kuwa linaifadhili shule hiyo.
Akipinga uamuzi huo, Sheikh Abdullahi Gudo wa Baraza la  Maimamu na Wahubiri Kenya CIPK amesema uamuzi huo wa mahakama ni ukiukwaji wa wazi wa haki za wasichana  wa Kiislamu ambao wanafuata mafundisho ya dini yao. Ameongeza kuwa Wizara ya Elimu Kenya imeidhinisha uvaaji wa Hijabu shuleni na hivyo shule zote zinapaswa kufuata agizo la serikali ya Kenya.../mh

1455118

Kishikizo: kenya waislamu hijabu
captcha