IQNA

Idul Fitr

Wananchi wa Iran kusherehekea Idul Fitr Jumatano 10 Aprili  

20:32 - April 09, 2024
Habari ID: 3478659
IQNA – Hilali ya mwezi wa Shawwal imeandamana leo jioni nchini Iran na kwa msingi huo Jumatano Aprili 10 2024 itakuwa Mosi Shawwal 1445 Hijria Qamaria na siku kuu ya Idul Fitri.

Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imesema , kwa mujibu wa ripoti zilizopokelewa kutoka kwa makundi ya wataalamu na waangalizi wa kutegemewa kutoka sehemu mbalimbali za Iran, mwezi wa Shawwal umeandama wakati wa kuzama kwa jua Jumanne tarehe 9 Aprili 2024 sawa na tarehe 29 Ramadhani 1445 Hijria na kwa msingi huo  Jumatano Aprili 10, 2024, itakuwa siku ya kwanza ya Shawwal 1445 na siku kuu ya Idul Fitr.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei anatazamiwa kuswalisha sala ya Idul Fitr jijini Tehran katika Uwanja wa Sala wa Imam Khomeini (MA).

Baadhi ya wasomi wa Kiislamu hutegemea hesabu za unajimu ili kubaini mwanzo wa miezi ya mwandamo huku wengi wao wakiamini kuwa inatosha kuona mwezi mwandamo kwa jicho au vifaa vya kisasa kama teleskopu.

Nchi nyingine nyingi za Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Iraq, Morocco, Oman, Pakistan, na Libya, pia zinatazamiwa kuadhimisha siku kuu ya Idul Fitr Aprili 10.

4209428

Kishikizo: idul fitr shawwal
captcha