IQNA

Rais wa Syria atoa msamaha kwa wote ambao hawajahusika na mauaji

16:16 - September 16, 2019
Habari ID: 3472131
TEHRAN (IQNA) - Rais Bashar al-Assad wa Syria ametoa amri ya msamaha au kupunguza vifungo kwa watuhumiwa ambao hawakufanya jinai kama za kuua watu nchini humo.

Kwa mujibu wa amri hiyo, msamaha huo wa Rais Assad utawahusu watu ambao walitenda makosa kabla ya tarehe 14 Septemba mwaka huuu. Aidha magaidi hawajumuishwi kwa aina yoyote katika msamaha huo wa rais wa Syria. Kadhalika askari ambao walijitenga na jeshi, iwapo watarudi jeshini hadi kabla ya mwezi Januari mwakani, nao watasamehewa. Tangu kulipoibuka mgogoro wa Syria, serikali ya Damascus imekwishachukua hatua za kuwaachilia huru watu 3952. Mgogoro wa Syria uliibuka kuanzia mwaka 2011 baada ya nchi hiyo ya Kiarabu kuvamiwa na makundi ya kigaidi na ukufurishaji yanayoungwa mkono na Saudi Arabia, Marekani, Israel, Imarati na washirika wao kwa lengo la kuleta mlingano katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) kwa maslahi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Hivi sasa jeshi la serikali ya Syria linakaribia kuwashinda kikamilifu magaidi ndani ya nchi hiyo. Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Walid al Muallem, amesema kuwa nchi yake itaendelea kuliunga mkono Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA). Al-Muallem ameyasema hayo leo alipokutana na Pierre Crinbull, Kamishna Mkuu wa shirika hilo ambapo wamejadili masuala muhimu yanayohusiana na matukufu ya taifa la Palestina na kusisitiza kuwa, licha ya Syria kuwa katika vita dhidi ya ugaidi, lakini inaunga mkono kikamilifu matukufu ya taifa la Palestina kama ambavyo inapigania kurejeshwa haki zilizoghusubiwa na utawala haramu wa Kizayuni.

3469414

captcha