IQNA

Utawala wa Israel wawazuia wabunge wawili wa Marekani kuingia Palestina

12:50 - August 16, 2019
Habari ID: 3472086
TEHRAN (IQNA)- Utawala haramu wa Israel umewapiga marufuku wabunge wawili wa chama cha Democrat nchini Marekani Rashida Tlaib na Ilhan Omar kuingia ardhi za Palestina.

Uamuzi huo uliotangazwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa kibaguzi wa Israel, Tzipi Hotovely, na unakuja kufuatia kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Uamuzi huo wa utawala haramu wa Israeli umesababishwa na pendekezo kutoka kwa rais wa Marekani Donald Trump.

Wizara ya Mambo ya ndani ya utawala wa Kizayuni wa Israeli ndio ilitangaza rasmi kuwa wabunge hao wawili kutoka Marekani hawataweza kuingia Palestina. Utawala haramu wa Israel umezingira ardhi zote za Palestina na hivyo unaweza vizingiti na vizuizi utakavyo kwa wageni wote wanaotaka kuingia katika ardhi hizo.

Utawala haramu wa Israel umeamua kuwawekea vikwazo vya usafiri wabunge wawili wa chama cha Democratic nchini Marekani baada ya Rais Trump kuiomba nchi hiyo kuwapiga marufuku.

"Itaonesha udhaifu mkubwa" ikiwa Israel itawaruhusu Ilhan Omar na Rashida Tlaib kuzuru taifa hilo, " Donald Trump alisema.

Wawakilishi hao wa Democrat ni wakosoaji wakubwa wa utawala wa Rais Trump na utawala dhalimu wa Israel, huku wakiunga mkono viguvugu la kimataifa kususiwa kwa Israel maarufu kama BDS kutokana na utatili wa utawala huo dhidi ya Wapalestina.

Wabunge hao wawili wa Democrat ni kati ya wabunge wanne wa Marekani ambao walidhalilishwa na Rais Donald Trump.

Hivi karibuni, Trump aliwatukana matusi ya kibaguzi wabunge wanawake wa chama wa Democrat katika Kongresi ya Marekani kwa kuwaambia, wao si Wamarekani na kuwataka warudi nchi walizotoka.

/3469167/

captcha