IQNA

Safari ya Mflame Salman wa Saudia nchini Bahrain na kuuhami utawala wa Aal Khalifa

13:54 - April 04, 2019
Habari ID: 3471898
TEHRAN (IQNA)- Mfalme Salman Bin Abdulaziz wa Saudi Arabia ameitembelea Bahrain katika safari fupi na kufanya mazungumzo na mfalme wa nchi hiyo Hamad bin Isa Aal Khalifa.

Safari ya Mfalme Salman nchini Bahrain Jumatano ilidumu kwa muda wa masaa matatu tu na kwa upande wa pili safari hiyo haikutarajiwa na ilifanyika  baada ya safari ya siku sita ya Mfalme Salman nchini Tunisia.

Kimsingi ni kuwa, kutokana na kuwa utawala wa Aal Khalifa ni tegemezi kwa utawala wa Aal Saud, inatarajiwa kuwa watawala wa Bahrain watakuwa ni watiifu na ni watumwa wa sera za Saudi Arabia. Hapa ndipo tunapoona tafauti zilizopo baina ya utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain na utawala wa ukoo wa Aal Thani nchini Qatar. Uhusiano wa Saudi Arabia na Qatar ummeingia dosari na umejaa uhasama kutokana na kuwa, ukoo wa Aal Thani hauko tayari kutii na kuufuata kibubusha ukoo wa Aal Saud na badala yake umeamua kufuata sera huru na za kujitegemea.

Ikumbukwe kuwa, Mnamo Machi 14 mwaka 2011, katika fremu ya 'Ngao ya Peninsula", Saudi Arabia iliingiza wanajeshi wake nchini Bahrain katika hatua ambayo wananchi wa nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi waliitaja kuwa ni ukiukwaji wa wazi wa mamlaka ya kujitawala nchi yao ni pia ukiukwaji wa msingi wa kanuni za kimataifa wa kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine.

Utawala wa Aal Khalifa mnamo Februari 14 mwaka 2011 ulikumbwa na mwamko wa wananchi. Watu wa Bahrain wana matakwa halali kabisa na wamekuwa wakiyabainisha kwa njia za kiraia na za amani na wanataka mabadiliko katika mfumo wa kisiasa ambao sasa unasimamiwa na ukoo wa Aal Khalifa. Lakini ukoo wa Aal Khalifa uliomba msaada wa Aal Saudi katika kukabiliana na mwamko wa Wabahrain kutokana na kuwa, aghalabu ya raia wa nchi hiyo wanatafuatiana kimadhehebu na koo hizo mbili zinazotawala kiimla. Kwa msingi huo koo hizo mbili zimeshirikiana katika kukandamizwa maandamano ya amani ya Wabahrain na ukandamizaji huo ungali unaendelea kwa mwaka wa tisa sasa.

Ni kutokana na mwamko huo ndio ukoo wa Aal Saud ukategmea Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi ili kutumia  muafaka wa kijeshi wa 'Ngao wa Peninsula' ili kuingia kinyume cha sheria nchini Bahrain. Hatua hiyo inakika sheria kwa sababu hatua ya  kijeshi katika fremu ya 'Ngao ya Peninsula' inapaswa kuchukuliwa tu wakati mojawapo ya nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi inapovamiwa na dola ajinabi. Hii ni katika hali ambayo mwaka 2011 Bahrain haikuvamiwa kijeshi na dola lolote kutoka nje ya baraza hilo.

Kwa msingi huo, ukoo wa Aal Saudi unahusika katika jinai zote ambazo zimetendwa na ukoo wa Aal Khalifa dhidi ya watu wa Bahrain katika kipingi cha miaka minane iliyopita. Kwa mtazamo huo wa ushikiriano katika jinai, kauli ya Mfalme Salman katika mkutano wake na Mfalme Hamad Bin Isa Aal Khalifa kuwa uhusiano wa Saudia na Bahrain ni wa  'kudugu' ni sahihi lakini miongoni mwa wananchi waliowengi nchini Bahrain kauli hiyo si sahihi kwani wanautazama utawala wa Saudia kama utawala ghasibu.

3800850

captcha