IQNA

Sudan yaanza ukarabati wa nakala za kale za Qur'ani

15:48 - February 17, 2019
Habari ID: 3471844
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Sudan imeanza mradi wa kitaifa wa kukarabati nakala za kale za Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa taarifa, shirika la uchapishaji linalojulikana kama Africa House for Printing the Glorious Quran limeanza mradi huo mnamo Februari 10.

Katika mradi huo, nakala zote za Qur'ani na misahafu inayohitaji ukarabati itakusanywa kutoka katika misikiti, madrassa na vituo vya kufunza Qur'ani pamoja na majumba ya watu binafsi kote Sudan.

Mohammad Abdulqadir wa kituo cha Qur'ani cha Darul Mushaf Al Afriqiya ametoa wito kwa raia, wanaharakati wa Qur'ani na wanafunzi wa madrassah kushirikiana katika mpango huo wa kitaifa wa kukusanya na kukarabati nakala za kale za Qur'ani Tukufu.

Shirika la uchapishaji la Africa House for Printing the Glorious Quran lilianzishwa mwaka 1415 Hijiriya Qamarai mjini Khartoum, Sudan.

Kati ya majumu ya shirika hilo ni uchapishaji wa nakala za Qur'ani kwa kuzingatia mbinu za qiraa zilizo barani Afrika na kuhimiza utafiti kuhusu Qur'ani Tukufu.

/3789259

captcha