IQNA

Mahakama Austria yabatilisha uamuzi wa serikali kufunga misikiti

21:20 - February 15, 2019
Habari ID: 3471842
TEHRAN (IQNA)- Mahakama nchini Austria imebatilisha uamuzi wa serikali kufunga misikiti sita ya jamii ya Waarabu nchini humo.

Katika taarifa Alhamisi, Umit Vural, mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Austria (IGGO) amesema mahakama katika mji mkuu, Vienna, imebatilisha uamuzi wa serikali kufunga misikiti sita.
Mwaka jana, serikali ya mrengo wa kulia ya Kansela Sebastian Kurz ilitangaza uamuzi wa kufunga misikiti saba na kuwatimua nchini humo Maimamu 10.
Kurz alisema uamuzi huo ulikuwa sehemu ya kukabiliana na kile alichokitaja kuwa 'Uislamu wa Kisiasa.'
Msikiti wa Jumuiya ya Kiislamu-Kuturuki Austria (ATIB) ambao nao ulikuwa pia umefungwa ulifunguliwa tena mwezi Juni mwaka jana baada ya kutumiza masharti.
Nchini Austria kuna takribani Waislamu 600,000 ambao aghalabu wana asili ya Kituruki.
Mwaka jana Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki alimkosoa Kansela Sebastian Kurz wa Austria kufuatia uamuzi wa serikali yake kufunga misikiti na kuwatimua maimamu.
Nina wasi wasi kuwa hatua ambazo kansela wa Austria amechukua zitapelekea dunia kukaribia vita vya msalaba na hilali," alisema Erdogan katika dhifa ya futari mjini Istanbul akiashiria uwezekano wa kuzuka vita baina ya Waislamu na Wakristo katika uga wa kimataifa.

3790240

captcha