IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Utawala wa Marekani ni nembo ya ushari

8:17 - February 09, 2019
Habari ID: 3471834
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, utawala wa Marekani ni nembo ya ushari, utumiaji mabavu, kuanzisha migogoro na kuzusha vita.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo Jumatano mjini Tehran alipokutana na makamanda na hadhara ya wafanyakazi wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kiapo cha utiifu cha kihistoria kwa Imam Khomeini mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran miaka 40 iliyopita.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa madhali utawala wa Washington ungali unafanya harakati kwa misingi ya ushari, kuingilia mambo ya nchi nyingine, hiyana na mambo machafu, nara ya “Mauti kwa Marekani” haitoacha kutoka katika vinywa vya wananchi wa taifa lenye nguvu la Iran. Aidha Kiongozi Muadhamu amebaini kuwa, nara ya 'Mauti kwa Marekani' haiwalengi wananchi wa Marekani bali huwa inawalenga watawala wa nchi hiyo ambao hivi hasa Rais Donald Trump, mshauri wake wa usalama wa taifa John Bolton na waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kwa kuwa macho wananchi na kwa mahudhurio ya watu wenye mitazamo tofauti maadhimisho ya mwaka huu ya 22 Bahman (Februari 11) ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yatakuwa makubwa na ya hamasa zaidi ikilinganishwa na ya huko nyuma.

Ayatullah Khamenei amesema kuwa, mahudhurio makubwa ya wananchi katika maandamano ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiisamu “yamekuwa yakimvunja adui na kumuogopesha” na kulihesabu hilo kuwa ishara ya mahudhurio ya wananchi katika medani na kudhihirika azma na umoja wa kitaifa.

3467884

captcha