IQNA

Wiki ya Kitaifa ya Qur'ani nchini Algeria

11:00 - December 07, 2018
Habari ID: 3471763
TEHRAN (IQNA)- Awamu ya 20 ya Wiki ya Qur'ani Tukufu nchini Algeria imefanyika huku kukitolewa wito wa kuhakikisha watoto wanajifunza Qur'ani.

 

Wiki ya Qur'ani huandaliwa maeneo yote ya nchi hiyo wakati huu kila mwaka chini ya usimamizi wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini Algeria.
Katika ujumbe wake kwa munasaba wa WIki ya Qur'ani, Rais Abdulaziz Bouteflika wa Algeria ametoa wito wa kuwepo jitihada maalumu za kuhakikisha watoto na vijana nchini humo wanajifunza Qur'ani na Sunnah.
Wiki ya Qur'ani Algeria imejumuisha mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani, tajwidi na tafsiri na pia warsya zilizopewa jina la "Utiifu kwa Qur'ani."
Algeria ni nchi iliyo katika eneo la kaskazini mwa Afrika na asilimia 99 ya wakaazi wake ni Waislamu.

3769387

captcha