IQNA

Nakala ndogo zaidi ya Qur’ani katika maonyesho nchini Uturuki

22:44 - October 19, 2018
Habari ID: 3471712
TEHRAN (IQNA)-Moja ya nakala ndogo zaidi za Qur’ani duniani imewekwa katika maonyesho katika mji wa Kusadasi, wilayani Aydin nchini Uturuki.

Nakala hiyo ya kipekee ya Qur’ani ni kati ya vitu vya umbo dogo vinavyoonyeshao katika maonyesho hayo ya kipkee.

Nakala hiyo ndogo ya Qur’ani iliandikwa kwa mkono na Necati Korkmaz ambaye ni Mturuki pekee mwenye uwezo wa kuandika kaligrafia kwa mtindo wa Gubari.

Nakala hiyo ya Qur’ani imetajwa kuwa una ukubwa wa chini ya sentimeta moja na iliandikwa katika kipindi cha miaka mitatu.

Necati Korkmaz anasema aghalabu  alifanya kazi hiyo ya kipekee wakati wa usiku. Aidha anasema amewahi kuandika majina 99 ya Allah katika ndengu moja na Bismillahi Ar Rhamani Ar Rahim katika unywele. Uandishi huo unatumia kalamu maalumu kwa kutegemea hadubini mikroskopu.

3467014

captcha