IQNA

Mwanamke wa Kwanza Mwislamu katika Bunge la Senate nchini Australia

23:15 - August 15, 2018
Habari ID: 3471629
TEHRAN (IQNA)- Muastralia mwenye asilia ya Pakistan, Bi, Mehreen Faruqi amekuwa mwanamke wa kwanza Mwislamu kuteuliwa kuwa senata katika Bunge la Senate la Australia.

Bi. Faruqi wa Chama cha Kijani (Green Party) ameteuliwa kuwakilisha jimbo la New South Walesna amesema atatumia nafasi yake kuhakikisha kuwa Australia inakuwa na mustakabali mwema wenye kuhehsimu watu wa kaumu mbali mbali.

Bi. Faruqi alihamia Australia mwaka 1992 kutoka Pakisan na ana shahada ya uzamivu katika uhandizi wa mazingira. Hii ni mara ya pilu kwa mwanasiasa huyo kupanda ngazi za kisiasa baada ya kucaghuliwa katika bunge la jimbo mwaka 2013. Anasema akaiw ambunge alikumbana na ubaguzi si kwa ajili ya kazi zake lakini kutokana na asili yake na rangi ya ngozi yake. Amewakosoa vikali wapinzani wake hasa mbaguzi Fraser Anning na kusema ana fahari kuwa ni mhajiri Mwislamu na sasa yeye ni seneta.

3738924/

captcha