IQNA

Vizingiti vya Saudia vyawazuia Waqatar kutekeleza Ibada ya Hija

14:53 - August 12, 2018
Habari ID: 3471626
TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa Qatar hawataweza kutekeleza Ibada ya Hija kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na idadi kubwa ya vizingiti ambavyo vimewekwa na utawala wa Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa taarifa Saudia imewekea mashirika ya Qatar vizingiti vingi na baada ya msimu wa Hija kuwadia imekuwa vigumu kwa Waqatar kutekekelza ibada ya Hija.

Gazeti la Arrayah la Qatar limeandika kuwa wakuu wa Saudia wameingiza masuala ya mzozo wa kisiasa katika ibada ya Hija. Mashirika ya Qatar yanasema kutokana na vizingiti hivyo hakuna tena muda wa kutosha wa kuandaa safari, makazi, malazi na huduma za afya za wanaopanga kutekelaza ibada ya Hija. Aidha usalama wa mahujaji wa Qatar haujadahminiwa hasa kwa kuzingatia kampeni iliyoanzisha Saudia dhidi ya watu wa Qatari.

Ikumbukwe kuwa tarehe 5 Juni mwaka 2017, Saudia ilikuwa ya kwanza kukata uhusiano wake wote na nchi jirani ya Qatar na siku hiyo hiyo ikafuatiwa baadaye na Bahrain, Imarati na Misri. Nchi hizo zilidai kuwa Qatar inaingilia masuala yao ya ndani na pia ina uhusiano na makundi yaliyotajwa na nchi hizo nne kuwa ni ya kigaidi kama ambavyo ziliitaka pia ivunje uhusiano wake na Iran na pia Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas.  Aidha nchi hizo ziliituhumu kanali ya televisheni ya Al Jazeera inayomilikiwa na Qatar kuwa ni ya kichochezi na zimetaka ifungwe mara moja.

Qatar imepinga tuhuma zote hizo huku ikikataa kutii masharti iliyopewa ili uhusiano wa kawaida kurejea. Wakuu wa Doha wanasitiza kuwa ina uhuru wa kujiamulia mambo yake na kwa msingi huo imekataa kutii matakwa ya nchi hizo za Kiarabu jambo ambalo limepeleka mgogoro baina ya nchi hizo za Kiarabuo uendelee kutokota hadi sasa. 

Saudia inatumia uenyeji wake wa maeneo matukufu ya Kiislamu kuwawekea vizingiti raia wa baadhi ya nchi ambazo inazozana nazo jambo ambalo limepelekea kuweo miito ya kuwepo usimamizi huru wa miji mitakatifu ya Makka na Madina.

3466521

captcha