IQNA

Wakimbizi Warohingya Wasema UN Imekataa Kuwatetea Wapate Uraia Wao Myanmar

10:49 - June 11, 2018
Habari ID: 3471552
TEHRAN (IQNA)- Wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya ambao wamekimbia ukandamizaji katika ardhi zao za jadi nchini Myanmar wamebainisha masikitiko yao baada ya Umoja wa Mataifa kushindwa kuwatetea wapate haki ya uraia.

Wakimbizi  Warohingya ambao wamepata hifadhi katika nchi jirani ya Bangladesh wamesema wamevunjwa moyo kufuatia mapatano yaliyotiwa saini na Umoja wa Mataifa ambapo takwa lao kuu, yaani uraia, halikuzingatiwa hata kidogo.

Jumatano iliyopita, Myanmar ilitia saini mapatano na mashirika ya Umoja wa Mataifa ambapo wakimbizi 700,000 Waislamu Warohingya  wataruhusiwa kurejea katika ardhi zao zao jadi.

Wakimbizi hao wanasema hawana matumaini kuhusu mapatano hayo kwani kwa miongo mingi wamezoea kusikia ahadi tupu za utawala wa kiimla wa Myamnar ambao unazidi kuwakandamiza Waislamu.

Mapatano hayo ya UN na Myanmar yanaandaa mazingira ya kurejea kwa hiari, na kwa usalama wakimbizi Warohingya walioko Bangladesh lakini haki ya uraia ya Waislamu hao imepuuzwa kabisa. Katika taarifa ya serikali ya Myanmar baada ya mapatano hayo, neno Rohingya halikutumiwa jambo ambalo linaashiria serikali hiyo ya Mabuddha  haiwatumbui Waislamu Warohingya kama jamii rasmi nchini humo. Taarifa hiyo imewataja tu  kama ‘watu waliofurushwa makwao.’

Jinai kubwa wanazofanyiwa Waislamu hao na wanajeshi na Mabudha wa nchi hiyo  wenye misimamo ya kufurutu katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa Myanmar zilishika kasi tangu tarehe 25 mwezi Agosti mwaka 2017. Hadii sasa  jina hizo zimepelekea kuuliwa Waislamu zaidi ya elfu sita na kujeruhiwa maelfu ya wengine huku wengine karibu laki saba wakilazimika kuwa wakimbizi katika nchi jirani ya Bangladesh.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa uhalifu unaofanywa na Mabudha kwa himaya ya serikali nchini Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ni mauaji ya kimbari.

Zeid Ra'ad Al Hussein anasisitiza kwamba, kuna udharura wa kufika katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kufanya uchunguzi kuhusu ukatili unaofanywa na serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu.

3466027

captcha