IQNA

Wanaharakati waandamana Nigeria wakitaka serikali imuachilie Sheikh Zakzaky

21:09 - April 11, 2018
Habari ID: 3471461
TEHRAN (IQNA)- Wanaharakati wa Akademia katika Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Jumanne wameandamana wakitaka serikali imiachilie kiongozi wao aliye kizuzizini Sheikh Ibrahim Zakzaky huku aachiliwe huru mara moja.

Waandamanaji hao walikusanyika mjini Abuja wakitaka serikali imuachilie huru Sheikh Zakzaky kutokana na hali yake mbaya kiafaya.

Kingozi wa Wanaharakati wa Akademia katika Harakati ya Kiislamu ya Nigeria,  Malam Abdullahi Musa, amesema maandamano hayo ni ya 91 tokea Sheikh  Zakzaky  awekwe kizuizini 2015.

Itakumbukwa kuwa Sheikh Ibrahim Zakzaky akiwa na mke wake walitekwa nyara na Jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka 2015 wakati askari walipovamia kituo chake cha kidini huko katika mji wa Zaria jimboni Kaduna. Tokea wakati huo Sheikh Zakzaky na mkewe wamekuwa wakizuiliwa katika mojawapo ya vituo vya kijeshi vya nchi hiyo bila kufunguliwa mashtaka.

Uvamizi huo ulijiri baada ya Jeshi la Nigeria kudai kuwa wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria walikuwa na njama ya kutaka kumuua mkuu wa jeshi hilo, madai ambayo yalikanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo.Inakadiriwa kuwa Waislamu 1000 wasio na hatia waliuawa katika tukio hilo .

3465529

captcha