IQNA

Al Azhar yasisitiza kuhusu kuadhibiwa magaidi wa ISIS wanaorejea makwao

19:47 - February 13, 2018
Habari ID: 3471389
TEHRAN (IQNA)- Idara ya kupamabana na misimamo mikali katika Chuo Kikuu cha Al Azhar cha Misri imesema wafuasi wa kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) wanaorejea katika nchi zao wanapaswa kuadhibiwa kwa ajili ya jinai walizotekeleza.

Katika taarifa, idara hiyo ya Al Azhar imetangaza kuwa: "Kueneza klipu za video za  kundi la ISIS zinazoonyesha wapiganaji wa kike katika kundi hilo ni ishara ya kufeli  ISIS."

Taarifa hiyo imesema, "hivi karibuni kundi hilo lilieneza klipu yenye anuani ya "kutoka katika kitovu cha khilafa" ambapo  wapiganaji wa kike walionekana wakiwa pamoja na wapiganaji wa kiume na hilo ni jambo linaloonyesha kuwa kundi hilo la kigaidi haliwezi chochote ili uzushi na kupanga njama."

Al Azhar imesema hatua ya ISIS kuwalazimisha wanawake kuingia katika medani ya vita ni ishara ya kuendelea kushindwa kundi hilo.

Katika miaka ya nyuma ISIS ilikuwa inasisitiza kuwa wanawake hawapasiw kuenda katika mstari wa mbele wa vita na wanapaswa kubakia nyumbani tu kuwahudumia wanaume. Al Azhar imetoa wito kwa nchi ambazo raia wake, hasa vijana na wanawake, wameenda na kujiunga na ISIS ziwe na mipango kamili ya kuwaelimisha na kuwaondoa fikra zenye misimamo mikali ili waweze kuishi kwa amani na wengine lakini hilo lifanyike tu kwa sharti kuwa hawajahusika na jinai.  Aidha Al Azhar imesema watu kama hao wanapaswa kuadhibiwa kwa kosa la kujiunga na ISIS na wale waliotenda jinai kama mauaji na jinai zingine dhidi ya binadamu nao pia wanapaswa kuadhibiwa kwa mujibu wa sharia.

3690863

captcha