IQNA

Sayyed Hassan Nasrallah

Marekani ilitoa msaada kwa magaidi wa ISIS mjin al Bukamal, Syria

23:30 - November 21, 2017
Habari ID: 3471272
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Marekani imeilisaidia kundi la kigaidi la ISIS au Daesh katika mapigano ya hivi majuzi katika mji wa al Bukamal nchini Syria hatua ambayo inakinzana na madai ya Washington kwamba inapambana na ugaidi

Sayyid Hassan Nasrallah ambaye alikuwa akizungumzia ushindi wa Syria na waitifaki wake na kuangamizwa kundi la kigaidi la ISIS katika mji huo amesema kuwa, kukombolewa kwa mji wa al Bukamal ambao ulikuwa wa mwisho kutwaliwa na magaidi wa kundi la ISIS nchini Syria ni ushindi mkubwa.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa Marekani imelisaidia kundi la ISIS katika mapigano ya Bukamal kadiri ilivyoweza na kwamba iliwasaidia wapiganaji wa kundi hilo kwa kuwapa kivuniko cha anga, kuwapa taarifa za kiintelijensia na kiupelelezi juu ya maeneo ya jeshi la Syria, wapiganaji wa Hizbullah na washirika wao, kusimamia vita vya kielektroniki na kadhalika.

Aidha amesema Marekani pia iliwasafirisha kwa helikopta makamanda wa kundi la kigaidi na Kiwahabi la ISIS baada ya kipigo cha al Bukamal na kuwapeleka katika maeneo yanayodhibitiwa na wapinzani wa serikali ya Damascus.

Sayyid Hassan Nasrallah amesisitiza kuwa kukombolewa kwa Bukamal kuna maana ya kumalizika kabisa ISIS kama kundi la kijeshi na eti dola la Khilafa katika chini za Iraq na Syria lakini ametahadharisha kuwa wapiganaji wa kundi hilo wangalipo huku na kule katika maeneo mbalimbali ya Syria.

Kiongozi wa Hizbullah amesema ushindi dhidi ya kundi la Daesh ni ushindi wa maadili na thamani za Kiislamu dhidi ya ukatili na unyama wa magaidi wa Kiwahabi wanaoungwa mkono na Saudi Arabia na Marekani.

Jeshi la Syria, wapiganaji wa Hizbullah na washirika wao walifanikiwa kuukomboa mji wa al Bukamal ulioko kwenye mpaka wa nchi hiyo na Iraq kutoka kwenye makucha machafu ya kundi la Kiwahabi la ISIS Jumapili iliyopita.

Kuangamizwa ISIS

Kufuatia kutimuliwa kundi la ISIS kutoka miji yote lilolokuwa limeiteka Iraq na Syria, utawala bandia wa khilafa ya ISIS umesambaratika na kubakia katika makavazi ya historia. Mambo muhimu zaidi yaliyochangia katika kuanguka ya kusambatatika utawla huo bandia ni fatuwa ya kihistoria ya Ayatullah Ali Sistani ya kuanzishwa makundi ya kujitolea ya wananchi kwa ajili ya kupambana na kundi hilo la kigaidi, na irada na azma kubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia, Syria na makundi ya mapambano ya Kiislamu hususan harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

3665279/

captcha