IQNA

Wasichana Waislamu wanaovaa Hijabu shuleni Uingereza kusailiwa

18:38 - November 20, 2017
Habari ID: 3471271
TEHRAN (IQNA)_Wakaguzi wa shule nchini Uingereza wametakiwa kuwasaili wasichana Waislamu katika shule za msingi iwapo watapatikana wamevaa mtandio au vazi la Hijabu wakiwa shuleni.
Wasichana Waislamu wanaovaa Hijabu shuleni Uingereza kusailiwaAmri hiyo imetolewa na mkuu wa Idara ya Viwango vya Elimu Uingereza (Ofsted) ambaye pia ni mkaguzi mkuu wa shule, Bi. Amanda Spielman. Ametoa uamuzi huo wiki moja tu baada ya kukutana na wanaofanya kampeni za kupinga hijabu katika shule za Uingereza ambao walionekana kukasirishwa na ripoti iliyosema asilimia 20 ya shule 800 za serikali katika maeneo 11 ya England zimeorodhesha hijabu kama sehemu ya mavazi rasmi ya shule au unifomu, ingawa wenye kuvaa wana hiari.

Kufuatia uamuzi huo, Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Uingereza, Harun Khan amebainisha wasi wasi wake kwamba Ofsted imetangaza kuwalenga na kuwasaili wasichana wa shule wanovaa mtandio.

"Ujumbe wa wazi hapa kwa wanawake wote Uingereza wanaovaa hijabu ni kuwa wao ni raia wa daraja ya pili, "amesema Khan.

Aidha amebainisha masikitiko yake kuwa hivi sasa kubaguliwa wanaovaa hijabu ni sera nchini Uingereza. Amesema sera kama hivyo itakuwa na matokeo ambayo hayakukusudiwa huku akisisitiza kuwa wazazi Waislamu na watoto wao wana haki ya maamuzi na hawapaswi kupuuzwa

Waislamu ni takriabni asilimia 4.4 ya watu wote Uingereza na ni jamii ya waliowachache inayostawi kwa kasi zaidi.

3464470

captcha